Mambo 5 ya Kufahamu Kuhusu Baunsa (Mlinzi) wa Diamond Platnumz - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mambo 5 ya Kufahamu Kuhusu Baunsa (Mlinzi) wa Diamond Platnumz

SUALA ya ulinzi halina mjadala kwa watu maarufu kwani humuweka msanii kwenye nafasi nzuri zaidi ya usalama anapokuwa kwenye shughuli zake za kikazi. Ndiyo maana nyota wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amelitambua hilo na mara zote huwa anaambatana na baunsa wake, Mwarabu Fighter, ‘jitu’ la miraba minne lililojengeka misuli kwa ulinzi anapokuwa kwenye matukio yanayo mkutanisha na watu wengi.

Swaggaz linakusogezea mambo makubwa matano ambayo huwenda ulikuwa hujajui kuhusiana na baunsa wa Diamond Platnumz (Mwarabu Figther) kama tulivyofanya mazungumzo naye maeneo ya Mbezi Beach Africana jijini Dar es salaam.

MWARABU NI NANI
Anasema watu wengi wanadhani jina la Mwarabu ni jina la kazi kumbe ni jina lake halisi alilopewa na wazazi wake. “Jina langu kabisa naitwa Mwarabu Suleiman Mirundi hilo la mbele (Fighter) nililiweka baada ya kujikuta nafanya vitu vikubwa kwenye mlolongo wa maisha yangu niliyoyapitia pia nina mke na watoto wawili Sandra na Tariq,” anasema.

1. ALIWAHI KUPIGA DEBE UBUNGO
Mwarabu anasema kabla ya kukutana na Diamond, alikuwa anapiga debe kwenye kituo cha mabasi yaendayo mikoani, Ubungo huku akiendeleakufanya kazi ya ubaunsa kwenye matukio ya kiburudani katika Jiji la Dar es salaam.

“Pamoja na kufanya shughuli za ubaunsa kwenye ‘events’ mbalimbali kama vile Fiesta nilikuwa na shughuli zangu pale Ubungo, nilikuwa napiga debe kwenye mabasi ya mkoani.

“Kama wewe ni abiria unayekwenda Arusha ukifika Ubungo lazima ukutane na Mwarabu Fighter, nilikuwa nakikabidhiwa basi hata kuwe kuna ugomvi
namna gani lazima lijae, zaidi ya miaka kumi nimefanya kazi pale na nilikuwa na timu yangu kubwa inayokubalika mno,” anasema.

2. AUMINIFU WAMPA SHAVU
Anasema ni muda mrefu amekuwa akifanya kazi kama baunsa kwenye ‘events’ mbalimbali na huko ndiko alikutana na Diamond ambaye alikuja kumuhitaji kufanya naye kazi baada ya kukutana mara nyingi ambapo alivutiwa na utendaji kazi wake pamoja na uaminifu.

MSIBA WA NGWEA
Mwarabu anasema mara ya kwanza kumlinda Diamond Platnumz ilikuwa ni kwenye shughuli ya kuuaga mwili wa rapa, Albert Mangwea.


“Tulikaa kwa muda wa miezi kama mitano hivi, nikashangaa siku hiyo ananipigia simu, akaniambia twende Leaders Club ambako Ngwea alikuwa anaagwa, tukaaga pale tulipomaliza nikamsindikiza mpaka alipoishia mimi nikaondoka zangu,” .

“Nakumbuka ilikuwa mwaka 2012 kwenye Fiesta aliyokuja Rick Ross, walipaki basi lao ndani kabisa ya uwanja wa Leaders, kulikuwa na fujo sana, baada ya Diamond kutumbuiza nilikuwa mmoja ya mabaunsa waliomtoa jukwaani na kumsindikiza mpaka kwenye gari lake, akaondoka.

“Kumbe jamaa alikuwa ameniona, baadaye nikampa namba zangu na mimi nikachukua zake, nikawa namsumbua sana mwisho wa sikuakanikaribisha nyumbani kwake kipindi anaishi Sinza,” anasema.

3. APOKEWA VIZURI NA FAMILIA YA DIAMOND
Upendo ambao familia ya Diamond Platnumz walimwonyesha siku ya kwanza alipokaribishwa nyumbani kwa Chibu, hawezi kuusahau kwenye maishayake.

“Nilipofika nyumbani kwa Diamond nilimkuta yeye, mama, dada yake, Esma na mpiga picha wake, upendo walionionyesha siwezi kuusahau, walinipokea vizuri sana na hivyo ndiyo tunaishi mpaka leo hii,” anasema.

4. APIGA ‘DAY WORKER’ MIAKA MITATU
Anasema kutoka hapo, Diamond alikuwa akiwa anakwenda sehemu anampigia simu, wanakutana wanakwenda pamoja na baada ya tukio kuisha Mwarabu Fighter anarudi zake Ubungo.

“Akaniambia anataka kunipeleka kimataifa, anahitaji tusafiri mara kadhaa ili nijifunze kutoka kwa mabaunsa wanao walinda wasanii wengine wakubwa kama yeye na viongozi mashuhuri wanafanyaje, toka mwaka 2013 nikaanza kusafiri naye baada ya kujiridhisha akaja kunipa mkataba mwaka juzi, namshukuru sana Diamond siyo peke yake hata viongozi wa WCB, Babu Tale, Sallam Sk, Mkubwa Fella na wengine,” anasema Mwarabu.

5. APANGA KUUPA THAMANI UBAUNSA
Anasema amepanga kuipa thamani kazi ya ubaunsa kwani kwenye jamii kuna dhana mbaya iliyojengeka kuwa baunsa ni watu wakorofi, wezi, walevi nk.
“Kuna baunsa wachache ambao hawaitambui hii kama ajira, wanachukulia poa mwisho wa siku wahaharibu, huwezi kumlinda mtu ukiwa umelewa hivyo mimi najitahidi kuonyesha njia ili kazi hii izidi kupata heshima,” anasema Mwarabu.

- Mtanzania

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.