List ya Michepuko Iliyosababisha Diamond Kutoswa na Zari - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

List ya Michepuko Iliyosababisha Diamond Kutoswa na Zari

Habari za Diamond na Zari kuachana bado zinatawala kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wakiwa wameshtushwa kusikia kuwa couple iliyokuwa inapendwa na mashabiki zao imevinjika.

Huku sababu ya Zari kumwaga Diamond ikiwa ni wazi kabisa kuwa ni michepuko ambapo Zari ameweka wazi sababu juu iliyomfanya mpaka akafikia uamuzi wa kumuacha Baba watoto wake ni yeye kuzidisha kuchepuka.

Kwenye mahusiano yao yote kumekuwa na tetesi za Diamond kuwa na mahusiano na wanawake wengine, ingawa mara nyingi amekuwa akikataa na kudai ni uzushi lakini pia na Zari amekuwa akimsamehe na wawili hao huishia kurudiana.

Jambo hili lilimpelekea Zari kushindwa kuvumilia na kucharaza waraka katika mtandao wa instagram akieleza kuwa amechoshwa na tabia hiyo ya Diamond na anaachana nae ili kulinda heshima yake.

Baadhi ya michepuko ambayo inasemekana kuchangia kuvunja uhusiano wa Diamond na Zari ni hawa hapa:

Hamisa Mobetto
Hamisa anatajwa kuharibu uhusiano wa Diamond na Zari tangu mwaka jana alipojitokeza na kukiri kuzaa naye, na kuanzia hapo mahusiano ya Diamond na Zari yakaanza kuyumba ingawa alimsamehe lakini bado kulikuwa kuna mpasuko tayari.

Irene/ Officiallyn
Irene na Diamond wametajwa kuwa na mahusiano kwa muda mrefu sana tangu alipotokea kwenye video ya kwetu ya Rayvanny kama video queen kumekuwa na tetesi kuwa walikuwa wote South Africa at the same time akiwa na Zari na familia.

Shady
Huyu ni mwanamitindo kutoka nchini Rwanda tetesi za Diamond kutoka na Shady zilianza kusikika alitoa za kusafiri na kuelekea nchini Rwanda lakini zilipamba moto alipoenda Rwanda mwezi uliopita baada ya picha wakiwa pamoja kusambaa mtandaoni.

Mia
Mwezi uliopita kuna video ilisambaa mtandaoni ambayo ilimuonyesha Mia akiwa Madale ambapo baadae ilikuja kuonekana kuwa alienda pale na dancer wa Diamond ambaye alikuwa na mahusiano naye jambo ambalo Mia alikuja kulikana na kusema alienda pale na Diamond ambaye aliishia kulala naye.

Tunda
Uhusiano wa Tunda na Diamond ulikamata sana headlines ambapo inasemekana amekuwa mchepuko wake wa siku nyingi sana video iliyowaonyesha wakiwa pamoja ilisambaa mwezi uliopita.

Wema Sepetu
Wema na Diamond walitengeneza headlines wiki chache zilizopita baada ya kuonekana wakikumbatiana na kubusiana hadharani kwenye party huku kukiwa kuna tetesi kuwa wamerudiana.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.