Linah Amficha Mumewe Kisa Wivu, Aogopa Kuibiwa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Linah Amficha Mumewe Kisa Wivu, Aogopa Kuibiwa


Mwanamuziki diva wa Bongo Fleva, Linah Sanga ' Ndege Mnana' ameweka wazi hofu yake juu ya kuibiwa baba wa mtoto wake na wadada wa mjini (nyakunyaku) ndiyo sababu ya kupunguza kasi ya kumuweka mtandaoni kama jinsi ilivyokuwa awali.

Linah ameweka wazi hofu yake hiyo mbele ya kamer za eNEWZ wakati akifafanua tetesi za kupigwa kibuti na mfanyabishara huyo (Shabani Mchovu) ambaye wamefanikiwa kupata mtoto wa kike mwaka 2017.

Linah amesema kwamba yeye na Mchovu tayari wana takribani miaka miwili kwenye mahusiano na watu wengi wanafahamu kuwa ni wapenzi hivyo kumuanika mitandaoni ni kuzidi kuwatamanisha nyaku nyaku kumnyakua mpenzi wake ili kutaka kujua anakitu gani ambacho yeye anakipata kwa mpenzi wake huyo.

Aidha mwanamuziki huyo ambaye amerudi na ngoma mpya 'Same Boy' aliyomshirikisha Rachel Kizunguzungu amesema kwamba "mchumba wangu ni mtu ambaye anaheshima katika ofisi yake, hivyo siiwezi kumuingiza kwenye drama za kitoto au kumweka wazi haswa kwenye mitandao kwa kuwa nahofia kumshushia heshima yake lakini pia. Hayo ni mambo ya kitoto sana kuanika mapicha picha ukiwa na mpenzi wako".

Aidha ameweka sawa tetesi za kuchwa na kusema kwamba mapenzi na mpenzi wake hayajapungua wala hayajaisha na tangu wafanikiwe kupata.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.