Hizi ni Njia 4 za Kufanya Siku Yako Iishe kwa Furaha - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hizi ni Njia 4 za Kufanya Siku Yako Iishe kwa Furaha

Je unapoimaliza siku yako unakuwa katika hali gani? a) Hali ya wasiwasi na kutoridhika kwamba mambo yako hayajakamilika, b) kukasirishwa na mambo machache ambayo hayakwenda vizuri, c) Kuzidiwa na yote unayohitaji kufanya kesho au d) hali ya furaha kwa kutimiza yote uliyayapanga kufanya kwa siku hiyo?

Watu wengi wamekuwa wakiimaliza siku kwa uchovu na mawazo tele. Huku wakiwaza ni kwa namna gani watakidhi mapungufu yaliyojitokeza siku hiyo na kuifanya siku inayofuata kuanza vyema. Lakini husahau kwamba kuwaza sana yale yaliyoenda tofauti na malengo ya siku si vyema, bali kutafuta ufumbuzi wa namna ya kuyafanya kwa ufanisi zaidi.

Hizi hapa ni baadhi ya mbinu zitakazokusaidia kuimaliza siku yako ukiwa mwenye furaha.


Andika orodha ya mambo 10 mazuri yaliyotokea wakati wa mchana.


Watu wengi hupenda kuona mambo mengi zaidi yakifanyika kwa ukamilifu kila siku. Jambo ambalo hupelekea wao kuona kuwa mengi hayakwenda vizuri na kusahau yale yaliyo mazuri. Kuandika orodha ya mambo yaliyokuendea vizuri wakati wa mchana kutakufanya kuwa mwenye furaha zaidi.

Angalia au soma kitu ambacho kinaendana na ndoto zako.

unaposoma ama kuangalia vitu vinavyoendana na ndoto zako kutakuhamasisha na kukujenga zaidi kupambana ili kufikia lengo ulilojiwekea. Kupitia kusoma utaweza kupata mbinu mbalimbali za kukuwezesha wewe kujijenga zaidi na kupata kiu ya mafanikio.

Tafuta kinachokupa hofu na uchukue hatua kukirekebisha kabla ya kuanza siku nyingine.


hii ni njia mojawapo itakayokusaidia kuianza siku nyingine ukiwa na utulivu wa akili na maamuzi. Unapoamka ukiwa na hofu juu ya jambo fulani kunaweza kukakufanya ushindwe kukamilisha mambo mengine  na kukusababisha kutokufikia malengo uliyojiwekea. Hivyo kabla ya kuimaliza siku yako, jitahidi kutatua yale yanayokusumbua kabla hujaianza siku nyingine mpya.

Panga mambo utakayoyafanya utakapoamka asubuhi.


Wakati wa asubuhi huwa ni wakati mzuri ambao mwili pamoja na akili huwa na nguvu ya kufanya maamuzi. Ili usiichoshe akili yako mapema katika kuwaza mambo yasioyokuwa na msingi, basi wakati wa jioni unapomaliza siku yako panga vitu utakavyovifanya. Mfano panga nguo utakazovaa, chakula utakachokula pamoja na ratiba nzima ya siku inayofuata.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.