Hili Hapa Povu la Irene Uwoya Kwa Wanawake wa Bongo. - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hili Hapa Povu la Irene Uwoya Kwa Wanawake wa Bongo.

Kupitia kwenye ukurasa wa instagram wa muigizaji Irene Uwoya ameamua kuyaanika ya moyoni kuhusu wanawake ambao hawatoi ushirikiano kwa wanawake wenzao na hupenda kuona wenzao wakianguka au kufeli kimaisha ambapo hufurahishwa na jambo hilo.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Irene Uwoya ameandika;
“Hivi kwanin wanawake tunakuwa hatupendani???yani najiulizaga sana badala sisi tushirikiane ndo kwanza tunarudishana nyuma…mtu akifanya kitu kizuri au biashara ndo wa kwanza kuponda na kurudishana nyuma…yani unamskia mtu kabisa anakuponda mbayaaa afu hujawah ata kugombana na nae na pengine unamsaidiaga tu sana”

“Yani unashangaaa wanaokuunga mkono ni wanaume badala ya wanawake wenzako afu ukifanya mabaya ndo anakusifia balaaah ili uwendeleee kuharibuuu…!afu Sasa yeye akifanya lake anataka umuunge mkono anasahau yeye hakuwah kufanya hivyo!!!yani kuna mijitu ina rohooo daaahhh!!!”

Mimi Sasa hiv nimeamua si support mtu yeyote asie ni support na haina haja ya kuleana kabisa mtu asiye kuwa na humuimu kwenye maisha yako haina haja ya kuwa sehemu ya maisha yako atakurudisha nyuma tu!!!”

“Achana na watu wasio na faida wala mchango wowote kwenye maisha yako badilika!!!achana na marafiki wanao kushauri stareheee tu sikuzote…kaaa fikiri katika hao rafiki zako kuna siku atamoja walikushauri kitu cha maana cha kuingiza pesa??? au bataaa tuuu??? punguza watu wasio na mashiko kwenye maisha yako punguza marafiki wasio na faida” -Uwoya

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.