Gigy Money Mapenzi Moto moto na Mpenzi Wake Wamalizana Ugomvi Wao - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Gigy Money Mapenzi Moto moto na Mpenzi Wake Wamalizana Ugomvi Wao

Gigy Money Mapenzi Moto moto na Mpenzi Wake Wamalizana Ugomvi Wao
Mwanadada ambaye ni mwana-muziki na muuza sura kwenye video za Kibongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’, hivi karibuni amefunguka kwamba, hana matatizo tena na baba wa mtoto wake mtarajiwa aitwaye Mo Jay, na kwamba kila kitu kwa sasa wamekwisha kiweka sawa ambacho kilikuwa kinawafanya wagombane mara kwa mara.

Akichonga na Showbiz Xtra, Gigy aliongeza kuwa, wawapo wawili ‘tafaruku’ ndogondogo huwa hazikosekani, jambo ambalo lilikuwa linajitokeza kwao, lakini kwa sasa kila kitu kipo sawa na hawana tatizo kabisa.

“Sina shida yoyote na mpenzi wangu kwa sasa, kila kitu kipo sawa na yakiwepo ya kuzun-gumza kama tuna matatizo nitazu-ngumza huko mbele, lakini kwa sasa hakuna tatizo lolote,”
alisema Gigy.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.