Gigy Money Afunguka Kuchanganywa na Penzi ‘Unabeba Mimba na Dharau Anakufanyia’ - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Gigy Money Afunguka Kuchanganywa na Penzi ‘Unabeba Mimba na Dharau Anakufanyia’

Msanii wa muziki Bongo, Gigy Money amefunguka yale anayopitia katika mahusiano yake kwa sasa.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa ni mjamzito ametupa lawama zake nyingi kwa wanaume kwa madai ni watu wasioridhika katika mapenzi. Gigy Money ametumia Instagram kuandika ujumbe mrefu kueleza yaliyo moyoni;

Kiukweli Leo nina stress sana na ndio maana nimeona bora niseme kwani nachokiamini mm sio peke angu ninayo yapitia haya kuna muda unaweza ukakufuru Mungu kwa maneno ambayo kesho na kesho kutwa uwezi kuyarudisha kinywani katika makosa ambayo najua nimeyafanya nikupenda lakini kupenda sio dhambi nimepitia mengi sana kwenye Mapenzi kiasi chakufikia kupungua kimwili akuna kitu kibaya na kigumu kama kumuaminisha mtu unampenda unaweka nguvu na jitihada zako katika mapenzi kuna muda unawaza sijui niachie ngazi.

Walio karibu na mm wanaweza wakawa wanajua was baadhi ya mateso na utumwa wa mapenzi nilio wahi kupitia na still bado najiuliza kwann wanaume niwagumu kuonesha hisia zao za ukweli inashangaza mwanaume anaeza kuishi na ww pika pakua lakini anaempenda yuko mbali na upeo wa macho yake hicho kitu naamini wanawake wengi hawakiwezi ikiwa mm ni mmoja wao kama sikutaki nitakwambia in good way bila hata kugombana lakini mwanaume awezi kua muwaz na hii labda anapata kitu kidogo kwako yawezekana pesa,mavaz au umaarufu yote yanawezekana kiukweli natamani ningekua gigy yule ambae naweza kua na maamuzi yangu binafsi lakini nashindwa naumia mapenzi ni kitu ovyooooo .

Mara nyingi huwaga tunawapenda watu wenye uwezo wakawaida tukiamini mapenzi sio pesa ila wanaume wabongo wajeuri unabeba mimba dharau anakufanyia mwanamke wake wa nje atakuonesha kiukweli inauma ndio lakini naamini nihatua za maisha na ukuaji naamini nimedondoka hatua moja lakini naweza kuinuka hatua 8 Tanzania ni nchi inayoongoza kua na single mother’s sio wote baba wa watoto wamefariki wengi wetu huwaga tuna wakimbiza watoto wetu mbali na maisha na mateso tuliyo wahi kuyapitia kwa baba zao hakuna mtu anaeweza kunielewa ila mkiona mtu Ana type ivi ujue yanazidi hakuna kitu kibaya kama mtu akupendee kitu inauma sana.

Gigy Money ambaye ni hitmaker wa ngoma ‘Papa’ na kwa sasa ‘Mimina’ yupo katika mahusiano kwa muda mrefu na Mo J ambaye ni mtangazaji za Choice Fm.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.