Diana Afunguka Mpango wa Kwenda Kumuombea Lulu Gerezani - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Diana Afunguka Mpango wa Kwenda Kumuombea Lulu Gerezani

Elizabeth Michael 'Lulu' kushoto akiwa na Diana Kimaro

Mwigizaji wa filamu Bongo, Diana Kimaro, amesema anajipanga kwenda Gereza la Segerea jijini Dar kumuombea aliyekuwa swahiba wake, Elizabeth Michael ‘Lulu’ anayetumikia kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake, Steven Kanumba.

Akizungumza na gazeti hili, Diana alisema kuwa, zaidi ya mara tatu alishajipanga kwenda gerezani kumuona lakini hakuweza kufanikiwa kutoka na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake Ingawa kwa sasa amejipanga kwenda na wadada ambao kila mwisho wa mwezi wanaenda kuwapa Neno la Mungu wafungwa.

“Sio kwamba nipo kimya simkumbuki Lulu, hapana! Mwisho wa mwezi huu najipanga kwenda kumuona kuna wadada ambao huwa wanaenda kutoa Neno kila mwisho wa mwezi gerezani ndio nitaenda nao na ninajua wazi atafurahi sana,” alisema Diana ambaye ni muumini katika kanisa la Mchungaji Mwamposa.

-GPL

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.