Chuchu Hans Agoma Kumzalia Ray Mtoto Mwingine - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Chuchu Hans Agoma Kumzalia Ray Mtoto Mwingine

Ukizungumzia ‘kapo’ za mastaa ambao wamefanikiwa kuwa kwenye uhusiano na kubarikiwa kupata watoto wakiwa pamoja, huwezi kuacha kuwataja mastaa wakubwa wa sinema za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Chuchu Hans.

Wawili hawa ni kapo ambayo imefanikiwa katika hilo na uzao wao kuwa gumzo kila kona.

Chuchu ambaye amebarikiwa kupata mtoto wa kiume na Ray waliyempa jina Jayden, uhusiano wao huko nyuma ulikuwa wa kificho kikubwa, lakini kadiri siku zilivyosonga waliamua kuweka wazi.

Katika mahojiano ya Over Ze Weekend yaliofanyika ana kwa ana na Chuchu Hans, amezungumza mengi kuhusiana na maisha yao;

Over Ze Weekend: Unajisikiaje mtoto wenu kuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii?

Chuchu: Najisikia faraja na pia hakuna kitu kizuri kama mtu kumpenda mtoto wako. Kama mwanamke, lazima ujisikie faraja sana.

Over Ze Weekend: Kutokana na mtoto wenu kuwa kivutio, je hujabadili mawazo ya kutotaka kuzaa tena na kuolewa na Ray?

Chuchu: Msimamo wangu hauwezi kubadilishwa na mtoto. Kama nilisema hivyo, basi itaendelea kuwa hivyohivyo?

Over Ze Weekend: Kwa hiyo unaweza kwenda kuzaa tena na mtu mwingine na siyo Ray?

Chuchu: (kicheko)… mimi ningependa hapa nisiendelee kuzaa, lakini sijui huko mbele kitaka-chot-okea.

Over Ze Weekend: Kuna magumu yoyote uliyopitia kipindi cha ujauzito hadi kuzaa na ndiyo maana hutaki tena kuolewa?

Chuchu: Sitaki kuchuma ubaya kwa Ray, kuhusiana na malezi ya mtoto wake ni mtu ambaye anajali hilo na anampenda sana, kutoolewa ni uamuzi tu. Hata hivyo, kila mtu akili yake iko kwa mtoto, mambo mengine baadaye.

Over Ze Weekend: Mbona kuna tetesi kuwa unaishi nyumba moja na Ray?

Chuchu: Hilo sitaki kulizungumzia kabisa.

Over Ze Weekend: Kama wewe hutaki tena kuzaa na Ray, utajisikiaje akizaa mtoto na mwanamke mwingine?

Chuchu: Siwezi kujisikia chochote maana yeye ni mwanaume, anaweza kufanya lolote.

Over Ze Weekend: Inaonesha mtoto amepunguza kasi yako ya kufanya kazi zako za sanaa, unalizungumziaje hilo?

Chuchu: Hapana, nilitaka kumpa malezi ya kwanza kama mtoto, lakini sasa ameshatimiza mwaka, ninaweza kufanya kazi zangu na hata za mtu mwingine.

Over Ze Weekend: Hivi karibuni mwigizaji mwenzako, Blandina Chagula ‘Johari’ alifiwa na mama yake mzazi, Asha Chagula, lakini hukuonekana msibani, je, bado mna bifu?

Chuchu: (mshangao)… hapana! Nitaenda tu kumuona wala hatuna bifu.

Over Ze Weekend: Ninakushukuru sana Chuchu.

Chuchu: Asante na karibu. 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.