Chemical ' Najua Kupenda, Nahitaji Kubembelezwa' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Chemical ' Najua Kupenda, Nahitaji Kubembelezwa'

Msanii wa kike wa hip hop bongo Chemical, kwa mara ya kwanza amezungumzia maisha yake ya kimapenzi, kitu ambacho ni nadra sana kwa msanii huyo kufanya hivyo.

Akizungumza na team ya Planet Bongo ya East Africa Radio,  Chemical amesema yeye kama msichana ana hisia za mapenzi na anajua kupenda, ila anahofia kuumizwa hivyo hawezi nguvu nyingi kwenye masuala ya mapenzi.

“Unajua kuna mambo mengine tunayafanya kwenye muziki kuweza kuweka image nyingine, ila mi niko tofauti na niko real, ukisikiliza nyimbo zangu nyingi Chemical anajua kupenda, anataka kubembelezwa, mi msichana jamani, na mapenzi yapo, ila mimi nahisi nina vitu vini vya kufocus kiasi kwamba kwenye mapenzi sitii nguvu nyingi, sipendi moyo wangu uumie”, amesema Chemicla.

Chemical amefunguka hayo baada ya tetesi kuwa mpenzi wake alikuwa akiishi naye pamoja ambaye pia anayemsimamia, kutokea kutoelewana kiasi cha kususa kumsimamia kazi zake bila taarifa yoyote, licha ya kwamba alisaini naye mkataba.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.