Bella, Jack Pemba Warudiana Waonekana Wakila Bata La Nguvu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Bella, Jack Pemba Warudiana Waonekana Wakila Bata La Nguvu

Bella, Jack Pemba Warudiana Waonekana Wakila Bata
Licha ya msanii wa Bongo Fleva, Isabela Mpanda ‘Bella’ kuwahi kukiri kwamba amemwagana na aliyekuwa mpenzi wake, tajiri Jack Pemba ambaye ni Mbongo anayefanya biashara zake nchini Uganda, hivi karibuni wamezua gumzo baada ya kuonekana wakijiachia na kutupia picha mtandaoni wakiwa pamoja.

Bella ambaye kwa sasa ni mjamzito anayetarajiwa kujifungua muda wowote, yeye na Jack Pemba walizua gumzo kwa mashabiki na watu wao wa karibu waliokuwa wakijiuliza kwamba inawezekana mwanaume huyo ndiye baba kijacho wa Bella!

“Nawaona Bella na Jack Pemba wanajiachia tu huku Mbezi-Beach (Dar), wala hata hawaoni shida, sasa tunajiuliza huo ujauzito wa Bella ni wa Jack Pemba? Lakini Bella aliwahi kukiri kuwa ana mpenzi mwingine ambaye anafanya kazi benki, sasa hatuelewi maana hata baa aliyofungua Bella inasemekana amefunguliwa na huyo bwana,” alisema Mwanahawa Shaban ambaye ni jirani wa Bella.

Alipoulizwa Bella kama Jack ndiye baba mtoto wake mtarajiwa, alishikwa na kigugumizi akisema kuwa Jack Pemba alimtembelea tu kwenye baa yake ya Belas Bar iliyopo Mbezi-Beach, lakini hayo mengine hana majibu.

“Kuhusu mimba yangu kwamba ni ya Jack Pemba…sijui labda ni yake. Hapa amekuja kunitembelea tu kwenye baa yangu na kunisapoti pia,” alisema Bella.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.