Zari Afunguka Mazito Baada ya Diamond Kununua Mjengo Mpya - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Zari Afunguka Mazito Baada ya Diamond Kununua Mjengo Mpya

Mwanamuziki wa Bongo fleva Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amezidi kujidhihirisha kuwa yeye ni mkali baada ya Jana kuonyesha bonge la mjengo ambao utatumika kama makao makuu ya WCB.

Diamond ambaye ni mmiliki wa studio za Wasafi Classic Co. ambayo ilianza kama label ya muziki inayosimamia wasanii wakubwa wa Bongo fleva nchini kama Rayvanny, Harmonize, Lavalava, Rich Mavoko, Queen Darleen, Mbosso.

Wiki chache zilizopita kwa mara ya kwanza meneja wa Diamond, Babu Tale alidokeza kuwa kuna mpango wa kufungua stesheni ya redio na kituo cha televisheni ambavyo vitamilikiwa na Diamond. Lakini pia siku chache zilizopita alipokuwa nchini Kenya kwenye interview na kituo kimoja Diamond alithibitisha mipango hiyo ya kufungua television station na radio station hivi karibuni.

Siku ya Jana maneno hayo yalitimia kwani kwa mara ya kwwnza Diamond rasmi katambulisha mjengo mpya ambao utatumika kama makao makuu ya WCB na studio za redio na televisheni.

Baada ya habari hiyo njema na watu mbali mbali kumpongeza sana mzazi mwenza wa Diamond na mpenzi wake Zari the Boss lady alifunguka maneno mazito mtandaoni na kuandika mambo yafuatayo kwa Diamond:
Hongera Diamond sanaa kwa bidii na juhudi uliyonayo Allah akujaalie kwa mengine mazuri zaidi. Siku zote umekuwa mpiganaji wa kazi zako kwa kuwa njia pekee ya kuijenga familia ni kupiga kazi najua malengo yako Alhamdulilah!”.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.