Wastara: Wanaonisema Vibaya Siwezi Kuwachukia Mungu Ndio Anajua - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Wastara: Wanaonisema Vibaya Siwezi Kuwachukia Mungu Ndio Anajua

Msanii wa filamu nchini Wastara Juma Sajuki ambaye sasa anasumbuliwa na maumivu ya mguu na mgongo amefunguka na kusema kuwa watu ambao wanazungumza mabaya juu yake hawezi kuwachukia ila yeye amemwachia Mungu ndiye ajuaye yote.

Wastara amesema hayo wakati akiongea na EATV na kusema anawashukuru sana Watanzania na Rais Magufuli kwa moyo wao wa upendo na kujali matatizo yake kwani licha ya watu kumzungumzia kwa mabaya lakini bado wanaendelea kujitoa kwa msaada na kwenda kumuona jambo ambalo linazidi kumpa faraja.

"Nawashukuru na wao kwa changamoto wanayotoa kwa upande wangu nimeweza kujifunza kitu wakati wewe una tatizo lolote kuna watu hakuamini, inawezekana watu hao unaishi nao, unatembea nao au unawachukulia ni watu wema lakini mwisho wa siku wamevaa ngozi tu ya kondoo ndani yake wana mioyo ya chui. Kwa sababu mtu kusema anaumwa anaweza kuangaliwa na jamii nzima hivyo mtu yoyote anaweza kunitembelea na kunishuhudia sasa kivipi unaweza kuidanganya jamii.

Wastara aliongeza kuwa "Niseme tu wao waendelee kutoa changamoto kama ambavyo wameamua lakini wajue kwenye matatizo Mungu pia anahusika, anaweza kutoa mitihani, anaweza kukupima imani hivyo huwa hayaji kwa mtu mmoja leo yapo kwangu mimi lakini kesho yanaweza kumkuta mtu anayempenda yeye au yakamgusa huyo huyo mzungumzaji sijui atakuwa na wakati gani? Ila mimi namuachia Mungu yeye ndiye atajua atahukumu nini kwa watu ambao wanaongea 'negative' ila mimi siwezi kuwachukia ila naamini Mungu anajua fungu lao ni lipi" alisisitiza Wastara

Aidha Wastara amesema kuwa kwa sasa maandalizi yake ya safari kwenda kwenye matibabu yanaendelea vizuri na kama mambo yatakamilika huenda Jumapili ya tarehe 4 Februari 2018 ataanza safari kuelekea India kwa matibabu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.