Wanasheria Kumburuza Mhe. Lissu Mahakamani, Kwa Sababu Hii Hapa
![]() |
Cyprian Musiba |
Sasa Mwenyekiti wa Kampuni ya CZ International & Media Consultant LTD, Cyprian Musiba amesema kuwa yeye pamoja na baadhi ya wanasheria wamekusudia kumfikisha mahakamani Tundu Lissu kutokana na kauli zake alizotoa kwenye hotuba yake nchini Kenya wiki mbili zilizopita.
“Tundu Lissu aliutangazia Umma na dunia nzima kwamba Tanzania sasa si salama tena, nchi hii watu wanakufa hovyo hovyo kitu ambacho si cha kweli anapotosha ila Tanzania ni salama watu wanaabudu vizuri, wanajieleza vizuri ndiyo maana mimi nipo hapa najieleza kama kusingekuwa na uhuru wa kujieleza mimi nisingekuwa hapa. Tunampeleka mahakamani kwa sababu ameidhalilisha nchi yetu Kimataifa na Kitaifa na tunampa siku mbili tu atoe ushahidi wake na uthibitisho kwamba Tanzania siyo salama,“amesema Musiba jana January 15, 2018 kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
Hata hivyo, Musiba amesema wamempa Mhe. Lissu siku mbili kutoa uthibitisho wa kauli zake alizozitoa nchini Kenya huku akieleza kuwa matatizo yaliyopo nchini kwa sasa hayajaletwa na Serikali ya awamu ya tano kwani yalikuwepo toka serikali zilizopita.
Download App Yetu MPYA >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !
No comments
TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.