Vita ya Hamisa na Zari Yahamia Kwa Tunda, Fuatilia Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Vita ya Hamisa na Zari Yahamia Kwa Tunda, Fuatilia Hapa

Kwa muda mrefu wanamaa wawili Hamisa Mobeto na Zari The Boss Lady wamekuwa katika malumbano katika mitandao ya kijamii kuhusu nani kuwa juu zaidi ya mwenzie huku wote wakiwa wamezaa na bwana mmoja msanii mkubwa duniani Diamond Platinumz.

Mgogoro huu unaonekana kuendelea chini chini lakini safari hii inaonekana kuhamia kwa mtu mwingineambapo ni kati ya Hamisa Mobetto tena na Tunda ambae alishawahi kuwa video queen wa Diamond tena katika moja ya kazi zake.Siku kadhaa zilizopita kulikuwa na tetesi katika mtandao wa kijamii kuwa video queen huyo (Tunda) anatoka na msanii Diamond ingwa yeye mwenyewe alikanusha kabisa tetesi hizo.

Lakini mambo yanazidi kuwa moto tena hasa baada ya Tunda kuweka picha katika ukurasa wake wa instagram huku akiweka caption ambao inasemekana kuwa inalenga kutupia dongo kizani kwa Hamisa Mobeto.

Alipoweka picha hiyo ambayo ilimuonyesha yupo katika kibao kata cha rafiki yake, ambapo hata Hamisa alihudhuria, Tunda aliandika caption ya kusema “ebu angalia yule kinganganizi asiyejua maana ya kukataliwa na mwanaume‘ Maneno haya yanasemekana kumlenga Hamisa ingawa Tunda mwenyewe hakutaja jina la kinganganizi huyo.

lakini hata hivyo , inaonekana kuwa kwa muda sasa tunda amekuwa akiposti vitu vya kutaka kumuumiza roho Hamisa Mobeto , kwa mfano siku ya kuzaliwa kwa zari, tunda aliposti picha ya mwanamama huyo na kuandika “happy birthday mama T, wifi wa Taifa uliethibitishwa na Tbs,#nikiwamkubwanatakakuwakamawewe” Aliandika Tunda.

Ingawa mpaka sasa haijathibitika moja kwa moja lakini habari za chinichini zinasema kuwa tunda ana uhusiano wa kimapenzi na msanii Diamond. Lakini pia hata baada ya drama hizo zinazoendelea katika ukurasa wa instagram wa socialite Tunda , Hamisa hajataka kujibu chochcote kuhusu tuhuma hizo na wala kujibizana na mwanadada huyo.

Tunda na Hamisa wote kwa pamoja walishawahi kufanya kazi na Diamond katika moja ya nyimbo zake za mwaka uliopita wakiwa kama video queens katika wimbo wa Salome.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.