Video: Harmorapa Hajui Kama Ameingiza Faida Au Hasara - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Video: Harmorapa Hajui Kama Ameingiza Faida Au Hasara

Msanii wa muziki anayefanya vyema katika mitandao ya kijamii hasa Instagram, Harmorapa amejikuta akipata kigugumizi kuhusu kuingiza faida au hasara katika menejementi yake Sabuka Music.

Akiongea na Bongo5 msanii huyo anayehit na ngoma kadhaa kama vile ‘Shindu’ na ‘Mr.Kiki’ amedai kuwa yeye hafahamu kama ameingiza hasara au faida alipokuwa Sabuka Music.

“Baada ya Mr. Kiki kuna kazi zinakuja nitandondosha mzigo baada ya mzigo, harafu kwanza sipo katika menejiment mpya nafanya kazi zangu mimi kama mimi” amesema msanii huyo baada ya kuulizwa kama yupo katika manejement mpya.
Harmo akaongeza kuwa ni mpiango ya kazi tu kufanya kazi mwenyewe kwani ni jambo la kawaida ku-move kutoka hapo kwenda sehemu nyingine.

“Mimi nikizungumzia sana hapo kuhusu kama kuna faida ama hakuna faida hapo mimi sijui kiufupi yani. Nisema imeingiza faida hapo ama sijaingiza faida yoyote kipindi ambapo nipo sabuka muziki” Amesisitiza msanii huyo baada ya kuulizwa kuwa kuna tetesi kuwa amaingizia hasara menejimenti yake ya Sabuka.

Kuhusu kuhusika katika sakata la kumfukuzisha msanii mwezake katika menejimenti hiyo Harmo amedai kuwa yeye hakuhusika kumfukuzisha Kiloriti ila alikuwa na mambo yake.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.