Snura Afunguka Kuhusu Ishu ya Kukwapua Mpenzi wa Nisha - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Snura Afunguka Kuhusu Ishu ya Kukwapua Mpenzi wa Nisha

Msanii wa muziki Bongo, Snura amejibu stori za kumchukua aliyekuwa mpenzi wa masanii mwenzeye, Nisha.

Muimbaji huyo amelazimika kujibu hayo baada ya kuposti picha katika Instagram yake ya kijana akimtakia kheri ya siku ya kuzaliwa kwa ujumbe mzuri ambapo baadhi ya watu alidai kijana huyo aliwahi kuwa mpenzi wa Nisha.

Akizungumza na kipindi cha The Playlist cha Times Fm amesema mambo ya Instagram hayapaswi kuaminiwa na kuhusu kijana huyo hafahamu lolote kuhusu yeye na Nisha.

“Kwanza ukiniuliza kama yule alikuwa ni mwanaume wake hata sijui, hata sijawahi kumuona naye hata siku moja,” amesema Nisha.

Alipuliwa iwapo yeye ni Nisha ni marafiki wa karibu, alijibu; “Kwanza yule si rafiki yangu wa karibu maana kuna muda mwingine mnatengeneza vitu ili stori zenu zinoge ili mpate kuuza vizuri, hapana, yule si rafiki yangu wa karibu ni msanii mwenzangu tunakutana kwenye kazi basi!,”.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.