Siri ya Ndoa ya Dogo Janja na Uwoya Yafichuka Ukweli Huu Hapa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Siri ya Ndoa ya Dogo Janja na Uwoya Yafichuka Ukweli Huu Hapa

Siri ya Ndoa ya Dogo Janja na Uwoya Yafichuka Ukweli Huu Hapa
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni kama baba mlezi wa msanii Dogo Janja, Madee Senesa, ametoa sababu iliyowafanya wafanye siri kufungwa kwa ndoa ya Dogo Janja na Uwoya.

Akizungumza kwenye eNewz ya East Africa Television, Madee amesema walijua kuwa wawili hao ni maarufu, hivyo taarifa za ndoa yao ingewashangaza wengi na kuharibu mipango yote.

“Nilijua ni habari kubwa, ni habari ambayo ingeleta purukushani kwa wanahabari hata ndoa yenyewe isingefanyika, na hata wale ambao tumewaalika tulijua hawa wana marafiki zao ambao ni wana habari, hivyo tulichokifanya ni kutengeneza usiri wa ile shughuli, hata tuliowaalika tuliwaambia mnakuja hapa lakini simu zenu wekeni hapa, unangia unashuhudia tukio lakini hauna ushahidi wa kupeleka kwa wengine”, amesema Madee.

Madee ameendelea kwa kusema kwamba iwapo wasingefanya siri huenda wangetokea watu wa kuwashauri vinginevyo, na ndoa hiyo isingefungwa.

“Tungesema tuanze kuwaalika wangeanza kuwashauri usikubali kuolewa na yule au kumuoa huyu, ile ndoa ingekufa na sisi tungepata dhambi”, amesema Madee.

Mwezi Novemba mwaka 2017 msanii Dogo Janja na Irene Uwoya walifunga ndoa, jambo ambalo liliwashtua watu wengi, huku wengine wakisema ni kiki ya filamu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.