Sijaona Msanii wa Kunipa Changamoto - Ruby - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Sijaona Msanii wa Kunipa Changamoto - Ruby

Sijaona Msanii wa Kunipa Changamoto- Ruby
Msanii wa kike wa muziki wa Bongo Fleva, Ruby ameamua kuweka wazi kuwa kutokana na uwezo wake wa hali ya juu wa kucheza na sauti kwenye nyimbo zake amedai kuwa haoni msanii ambaye anampa changamoto.

Ruby baada ya kuulizwa kwenye kipindi cha Joto la Asubuhi cha E-FM kuwa ni msanii gani wa muziki wa kike hapa Tanzania anayempa changamoto alijibu jibu moja tu kuwa “SIJAONA”

Kwa upande, mwingine Ruby amesema kuwa kwa mwaka 2018 amejipanga kufanya mambo makubwa na kudai kuwa zile tofauti zake na baadhi ya vyombo vya habari ikiwemo kituo cha Radio cha Clouds FM kuwa zimeisha na sasa ni mwendo wa kazi tu.

“Kuna peace and love kwa watu ambao mwanzo tulikuwa hatupo ok first of all! second kilichobadilika ni akili yangu imebadilika katika utendaji kazi na jinsi ya kuishi pia na watu tofauti tofauti. Kujitathmini sio mbaya ili atleast ujue umefanya nini na nini hujafanya ili uweze kuaccomplish, ndio kitu ambacho mimi nimefanya, nimejaribu kuangalia kipaji changu kwa undani kinadeserve kuwa sehemu na kina stahili kupita njia gani ili kifike kinakostahili kufika, so nikahitaji kuwa na peace and love kwa kila mtu,“amesema Ruby.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.