Shamsa Ford Apigwa Marufuku Kutumia Mitandao ya Kijamii - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Shamsa Ford Apigwa Marufuku Kutumia Mitandao ya Kijamii

Staa wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford anadaiwa kupigwa stop kutumia mitandao ya kijamii na mumewe, Chid Mapenzi na kwa muda sasa haonekani hasa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram ambako aliwaaga kabisa mashabiki zake.

Chanzo kilieleza kwamba Chid Mapenzi alimpiga marufuku mkewe Shamsa kutumia mitandao ya kijamii kwa kuwa muda mwingi alikuwa akiutumia kwenye mitandao hiyo huku wakati mwingine akiambulia matusi kutoka kwa mashabiki zake jambo ambalo lilimchefua mumewe huyo na kuamua kumkataza.


Alipoulizwa Shamsa kuhusiana na suala hilo alikiri kwamba ni kweli mumewe alimtaka atoke kwenye mitandao ya kijamii kwa muda mpaka atakapomruhusu tena na hajui sababu za kukatazwa.

 “Kwa sasa naishi kwa amani sana maana nimepumzika na matusi ya mitandaoni siyaoni tena, sijui mume wangu aliona nini ila aliniambia nitoke mpaka atakaponiruhusu tena ndiyo nitarudi,” alisema Shamsa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.