Sanchez Amponza Thiery Henry, Je Ndiye Aliyemshauri Kuondoka Arsenal - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Sanchez Amponza Thiery Henry, Je Ndiye Aliyemshauri Kuondoka Arsenal

Alexis Sanchez anazidi kuleta habari nyingi tangu ajiunge Manchester United, na sasa mshambuliaji huyo wa Chile amemuweka katika wakati mgumu mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Thiery Henry.

Moja kati ya mambo ambayo Sanchez amesema wakati akijiunga na Manchester United ni ushauri alioupata kwa Thiery Herny ambapo Sanchez amedai kuzungumza na Henry kabla ya kuondoka.

Sanchez amesema Thiery Henry aliona ni sawa tu kwa yeye kuondoka Arsenal na Sanchez aliamua kufuata ushauri wa Thiery Henry na kuamua kuondoka Arsenal.

Mashabiki mtandaoni hii leo wengi wamekuwa wakimtupia Henry lugha chafu na wengine wakisema hawataweza kumtambua tena Thiery Henry kama legend wa timu ya Arsenal.

Mashabiki wengi wamedai kwamba Henry amekuwa akiwageuka mara nyingi na wengine wakikumbushia kwamba juzi tu aliwahi kumsifia Harry Kane wakati Tottenham ni wapinzani wao.

Sasa mashabiki wa Arsenal toka pande mbalimbali duniani wamekuwa wakiomba klabu ya Arsenal kuvunja sanamu la mchezaji huyo lililoko nje ya uwanja wa Emirates kwa kuwa Henry ni msaliti.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.