Ronaldinho Gaucho Atangaza Kustaafu Kucheza Soka - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ronaldinho Gaucho Atangaza Kustaafu Kucheza Soka

Ronaldinho Gaucho Atangaza Kustaafu Kucheza Soka
Mchezaji wa soka wa kimataifa wa Brazil Ronaldinho Gaucho leo ametangaza rasmi kustaa kucheza soka la ushindani baada ya kudumu katika soka la ushindani kwa zaidi ya miaka 15, Ronaldinho amefikia maamuzi hayo baada ya kucheza soka kwa muda mrefu na sasa anaamini inatosha.

Ronaldinho hadi anatangaza kustaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 37, amecheza vilabu zaidi ya saba toka aanze kucheza soka vikiwemo vilabu vya Paris Saint Germain ya Ufaransa, FC Barcelona na AC Milan.

Kama hufahamu Ronaldinho alizaliwa mwaka March 21 1980 Porto Alegre kwao Brazil na alinza kucheza soka katika timu ya vijana ya Gremio 1987, jina lake halisi ni Ronaldo lakini aliitwa Ronaldinho kutokana na kuwa na umbo dogo kuliko wote katika timu ya vijana aliyokuwa anacheza wakati huo akiwa na umri wa miaka 8.

Ronaldinho alianza kuingia kwenye headlines za vyombo vya habari akiwa na umri wa miaka 13, hiyo ni baada ya kufanikiwa kuipatia ushindi timu yake wa magoli 23-0 lakini magoli yote 23 alifunga yeye, hivyo nyota yake ya kuja kuwa staa wengi wanaamini walianza kuiona mapema. 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.