Mwanamke Amuuza Mwanawe wa Siku Tatu Siku ya Mwaka Mpya - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mwanamke Amuuza Mwanawe wa Siku Tatu Siku ya Mwaka Mpya

ITUI, KENYA: Mwanamke aliyejulikana kama Sarahi Kwamboka amepandishwa kizimbani kujibu tuhuma za kumuuza mwanae wa siku 3 siku ya mwaka mpya kwa dau la Shilingi 10,000 za Kenya.

Mtuhumiwa huyo ambaye ni Mama wa Watoto 3 alipandishwa kizimbani pamoja na anayedaiwa kumnunua mtoto huyo, Bi. Bernadette Musanya.

Korti ilielezwa kuwa Mtuhumiwa huyo wa kwanza alijifungua mtoto wa kike aitwaye Fridah Mutheu katika kituo cha afya cha Kanyangi siku ya Desemba 29, 2017 huko Kitui na siku 3 baadaye yaani siku ya mwaka mpya ndipo alimuuza kwa Bi. Musanya.

Wawili hao walikubali mashtaka ambapo mama huyo alidai amefanya hayo kutokana na umasikini unaomkabili na aliona atashindwa kumlea mtoto huyo pamoja na watoto wake wengine wawili.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.