Mama Uwoya Amjia Dogo Janja juu ni Baada ya Kupachika Mimba - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Mama Uwoya Amjia Dogo Janja juu ni Baada ya Kupachika Mimba

Staa wa sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya, Naima Uwoya akiongea jambo na anayedaiwa kuwa mume wake, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja.

Mwisho wa mjadala! Wakati mwanaye akidaiwa kupewa mjamzito, mama mzazi wa staa wa sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya, Naima Uwoya amefunga mjadala baada ya kutoa ya moyoni kuhusu ndoa ya binti yake huyo na msanii wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’, maelezo yaliyotafsiriwa kuwa ni kumtapika jamaa huyo.

Awali, kabla ya mama Uwoya kuzungumza na Ijumaa, kwenye mitandao ya kijamii kulienea picha na vipande vya video vikimuonesha Dogo Janja na Irene Uwoya wakiwa wanafunga ndoa huku wakipongezwa na wasanii wenzao.

Mbali na kupongezwa huko, Dogo Janja pia amekuwa akitamba waziwazi mara kadhaa kwamba anafurahia kumpata mweza wa maisha yake na Uwoya kwake ni mke bora.

Drama hizo zimeendelea kwa muda mrefu huku Dogo Janja akisisitiza kila mara kwamba Uwoya ni mkewe na hata meneja wake, msanii Hamad Ally ‘Madee’ naye amekuwa akipigilia msumari kuwa wasanii hao ni mke na mume, lakini Uwoya mwenyewe amekuwa akikanusha ishu hiyo.

Katika mahojiano na Ijumaa, mara kadhaa Uwoya alifunguka kwamba, picha na vipande hivyo vya video ni vya filamu yake mpya.

DOGO JANJA AZIDI KUSISITIZA

Kwa upande wake Dogo Janja amekuwa akibanwa kwa nyakati tofauti na kuzidi kung’ang’ania kwamba, Uwoya ni mkewe suala ambalo liliifanya timu ya gazeti hili kuingia kazini ili kubaini kama kweli wawili hao wanaishi pamoja au la.

Wakati timu hiyo ikiwa kazini, Uwoya alipatwa na majanga ya kufiwa na mumewe aliyezaa naye mtoto mmoja wa kiume, Hamad Ndikumana ‘Katauti’ kisha kusafiri kwenda nchini Rwanda kwa ajili ya mazishi.

Baada ya Uwoya kurejea Bongo, madai ya yeye kuoana na Dogo Janja yalizidi kuenea na nyepesinyepesi za sasa ni kwamba mwanadada huyo amenasa ujauzito wa Dogo Janja ambaye ni maarufu kwa jina la Janjaro.

Mbali na nyepesi hizo, hivi karibuni wawili hao walionekana kwenye harusi ya mwanamuziki na mwigizaji, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ambapo walitambulishwa kama mke na mume kwenye, jambo ambalo lilizidi kuzua gumzo kwa baadhi ya watu ambao bado wapo njiapanda juu ya suala hilo.


Irene Pancras Uwoya akiwa katika pozi.

IJUMAA KAZINI TENA

Kwa mara nyingine Ijumaa liliingia kazini ili kukubaini kama ni kweli wawili hao wameoana na wanaishi pamoja.

NYUMBANI KWA MAMA UWOYA

Gazeti hili liliweka ‘patroo’ nyumbani kwa mama Uwoya, Mbezi-Jogoo jijini Dar, lengo hasa likiwa ni kuzungumza na mzazi wa mrembo huyo ili kubainisha ukweli, maana kama ni Uwoya na Dogo Janja, wote wamekwishazungumza, lakini maelezo yao yanatofautiana.

Baada ya kutinga nyumbani hapo mama huyo hakuwepo badala yake gazeti hili lilikutana na dada wa kazi ambaye ndiye aliyebainisha kwamba mama mwenye nyumba hakuwepo.

IJUMAA LAMVUTIA WAYA MAMA UWOYA

Juhudi za kumtafuta mama huyo ziliendelea kwa Ijumaa kumvutia waya ambapo alipopokea simu na kuelezwa kila kitu kisha kutakiwa kusema anachokifahamu juu ya ndoa ya mwanaye huyo alikuwa na haya ya kusema:

“Ngojeni niwaambie, hakuna ndoa ambayo wazazi hawashirikishwi. Ndoa yoyote lazima wazazi wahusishwe na kushiriki.

“Ninachofahamu Irene ni mjane, mumewe ambaye sisi tunamfahamu ndiye huyo ambaye amekwishafariki dunia.

“Ninachojua mimi suala la kuoa au kuolewa, lazima wazazi wanashirikishwa kuanzia mwanzo hadi mwisho, kama tulivyoshiriki kwa mkwe wetu (Ndikumana).

AFUNGA MJADALA

“Irene ni mtu mzima, siwezi kumshikilia kwa chochote na hayo niseme tu kwamba ameamua kuyafanya mwenyewe.

“Kama yeye mwenyewe hajatupa taarifa kama kuna kitu kinaendelea, hatuwezi kumfuata na hatujui kama alishawahi kupewa talaka.

“Kwanza sisi wazazi wake siyo watu wa kwenda kwenye media (vyombo vya habari) na kusema hiki na hiki. Kama ingekuwa ni ndoa, mngeiona, mbona ndoa yake ile ya kwanza ya halali mliishuhudia kila kitu na mlituona? Hii ya sasa hatuitambui.

“Tunachojua mwanetu ni mjane. Kama ana ndoa, anaijua yeye, sisi hatuamini na wala hatumtambui huyo mtu anayeitwa Dogo Janja. Labda wanaigiza.”

TULIKOTOKA

Uwoya ambaye anafahamika kuwa ni mke wa ndoa wa Ndikumana kwani hajawahi kupewa talaka, aliwahi kudaiwa kuingia kwenye mapenzi na wanaume kadhaa kabla ya sasa kugandana na Dogo Janja. 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.