Kigwangalla Kutoa Fursa kwa Warembo na Vijana Wenye Mvuto - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Kigwangalla Kutoa Fursa kwa Warembo na Vijana Wenye Mvuto

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amefunguka na kusema kuwa mabinti warembo na vijana wenye muonekana mzuri wanaweza kutumika katika kazi za ukarimu na kusaidia kuleta sifa nzuri za wema na uungwana kwa wageni wanaotembelea Tanzania

Kigwangalla amesema kuwa kwa sasa wamekusudia kufanya mabadiliko makubwa katika sekta zote za huduma kwa wateja ili waweze kuwapa uzoefu wa kukumbukwa wageni mbalimbali wanaokuja nchini pamoja na kutangaza utamaduni wa nchi yetu. 

"Ukarimu ni utamaduni wetu. Tunahitaji kuutumia kibiashara. Lazima tubadilike, tuurejeshe kwa nguvu kubwa kwenye sekta zote za huduma kwa wateja na tuutumie kuwapa wageni wetu ‘experiences’ nzuri za kukumbukwa waende wakatusemee kwa wenzao huko kwao, wakawe mabalozi wetu. Tumedhamiria kuleta mabadiliko makubwa kwenye eneo hili"

Waziri aliendelea kusisitiza kuwa "Tanzania tuna wasichana warembo, kwa nini wasiajiriwe kwenye nafasi za kazi za ukarimu, tabasamu zao zikawa taswira ya wema na uungwana wetu kama Taifa! Tuna vijana imara, watanashati, wanaoweza kuwa taswira ya wema na uungwana wetu.

Majirani zetu wametumia hii, Leo imekuwa taswira ya nchi zao wakati sisi tunawajua hawana uungwana wala wema hata chembe...wanetengeneza taswira bora ya nchi yao. Hii haitushindi. Tuelekee huko sasa" alisema Kigwangalla

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.