Jibu la Mr. Blue Kuhusu Beef na Diamond na Mpango wa Kolabo - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Jibu la Mr. Blue Kuhusu Beef na Diamond na Mpango wa Kolabo

Msanii wa muziki Bongo, Mr. Blue amefunguka kuhusu kuwa na beef na Diamond na mipango ya kolabo.

Rapper huyo ambaye kwa sasa anatamba na ngoma ‘Mbwa Koko’ ameiambia FNL ya EATV kuwa kolabo na Diamond alishafanya mara mbili ila kama kuna uwezekano wanaweza kufanya tena ila kudhihirisha watu kuwa hawana beef kama inavyokuwa ikienezwa.

“Ni mtu nishashirikiana naye sio kitu cha kushangaza labda kusema haiwezekani lakini unajua siku zote mnapokuwa wasanii wakubwa kila mtu anakuwa yupo bize kwa upande wake lakini ikifanyika kolabo ya kati yangu na Diamond ni kitu kizuri kwa sababu tutaonyesha raia hatuna tatizo,” amesema Mr. Blue.

“Na kweli sina tatizo na Diamond, ni mdogo wangu namuheshimu, naheshimu hustle zake na amekuwa kama mfano kwa watu, hayo mambo mengine watu wasiyachukulie sana serious,”
amesisitiza.

Diamond ameshawahi kumshirikisha Mr. Blue katika ngoma yake inayokwenda kwa jina la kiss to the Lady, pia wote walishirikishwa na Marehemu Ngwea katika ngoma ‘BBM’.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.