Jacqueline Wolper: Hela ya Mwanaume Sio ya Kwako - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Jacqueline Wolper: Hela ya Mwanaume Sio ya Kwako

Msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amewataka wanawake kujishughulisha na kazi ili kuepuka kuwa tegemezi kwa wanaume.

Muigizaji huyo ameiambia FNL ya EATV kuwa fedha ya kupatiwa na mwanaume (kuhongwa) haiwezi kusaidia chochote bali kinachotakiwa ni wanawake kuwa za shunghuli zao binafsi.

“Wadogo zangu wa kike mwaka 2018 nitaendelea kuwatia hasira na ninawaambia hela ya mwanaume sio ya kwako, ukishachukua hela ya mwanaume fanya kitu chako usikubali kunyanyasika, mimi ni fundi cherehani ni hela yangu huwezi ukanitukana,” amesema.

“Unatakiwa upende hela yako, usitambe na hela ya mwanaume, usitambe na hela ya kuhongwa, fanya kazi yako ikupe heshima,” amesisitiza.

Licha ya Jacqueline Wolper kuwa msanii wa filamu pia ni mbunifu wa mavazi kupitia duka lake la House of Stylish.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.