Hemedy PhD Ajutia Maisha ya Zamani, 'Nlikuwa Nakula Mademu 5 Kwa Siku' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Hemedy PhD Ajutia Maisha ya Zamani, 'Nlikuwa Nakula Mademu 5 Kwa Siku'

Msanii wa Bongo Fleva na Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Hemedy PhD amekiri wazi kuwa mtindo wa maisha yake ya miaka ya nyuma kipindi anapata umaarufu yalikuwa ni mabaya kitabia hususani kwenye mahusiano huku akidai kuwa alikuwa anapenda sana mademu.

Hemedy amesema maisha hayo anayajutia hadi leo na amewaasa vijana wenzake kuwa wasiige mtindo huo wa maisha .

Mshindi huyo wa Shindano la Tusker Project Fame amedai kuwa kipindi cha nyuma alikuwa anatembea na wasichana hadi watano kwa siku.

“Sio kitu cha kujivunia kwa sasa hivi ila ni maisha ambayo nimeyapitia na nisingependa vijana wengine ambao wanaonisikiliza sasa hivi wafanye hivyo, Lakini mzee mimi nilikuwa nakula mpaka mashine (Wanawake) watano kwa siku.“amesema Hemedy PhD kwenye kipindi cha Playlist cha Times FM huku akieleza kuwa muda mwingine alikuwa anapangisha Hotel kwa ajili ya kazi hiyo tuu

“Ilikuwa ni panga pangua, Sometimes kabisa najenga kambi Hoteli mzee mimi nafumua tuu”
amesema Hemedy PhD .

Hata hivyo Hemedy PhD amesema kuwa mpaka sasa hakumbuki ni mademu wangapi alitembea nao ila anachokumbuka ni kuwa ametembea mademu wengi kipindi cha nyuma alivyoanza kupata umaarufu.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.