Harmorapa: Mimi Nikitua Kenya ni Staa Mkubwa Sana - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Harmorapa: Mimi Nikitua Kenya ni Staa Mkubwa Sana

Mwanamuziki wa Bongo fleva Harmorapa ametamba na kudai kuwa anapoenda nchi za jirani kama vile Kenya anakuwa mtu maarufu sana yaani wanamuona kama staa mkubwa sana.

Harmorapa alipata umaarufu mwaka jana baada ya kuingua kwenye gemu kwa gia za kufanana na msanii wa Bongo fleva kutoka label ya Wasafi Classic Harmonize na hata kuchukua jina lake lakini alizidinkujipatia umaarufu kwa tabia yake ya kupenda kiki kwa kila jambo atakalofanya.

Harmorapa alizidi kujizolea umaarufu baada ya kutangaza kwenye mitandao ya kijamii kuwa anampenda mrembo Wema Sepetu na kudai kuwa yuko tayari hata kumuoa lakini Wema alimtolea povu zito na kumkataza kumtaja taja na kumuongelea hovyo.

Harmorapa amerudi tena kwenye vichwa vya habari huku safari hii akidai kuwa yeye ni staa mkubwa zaidi nchini Kenya, Harmorapa amefunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5:

Unajua mimi mbali ya kuwa mwanamuziki lakini pia ni mfanyabiashara kwaiyo nilienda nchini Kenya kwa ishu za biashara zangu sasa si unajua mimi ni maarufu kule yaan nikitua tu watu wakajitokeza ambao ni wadau wakasema kwa nini tusifanye kitu fulani pia nikimaanisha kupiga shoo kwaiyo tukapiga shoo pale Kenya”.

Lakini pia Harmorapa amefunguka kuhusu dili lake na kampuni ya Swala ambayo ilikuwa inahusika na vinywaji jambo ambalo amekiri kuwa lile dili lilizingua na hivyo akaamua kuachana nalo kwa sababu habari zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa analipwa milioni 100 na kampuni hiyo ili kutangaza vinywaji vyao jambo ambalo amesema sio la kweli kwani amedai hajawahi hata kuiona hiyo pesa.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.