Dully Sykes Afunguka 'Diamond na Alikiba ni Biashara za Watu na Sitaki Kuingilia' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Dully Sykes Afunguka 'Diamond na Alikiba ni Biashara za Watu na Sitaki Kuingilia'

Msanii mkongwe wa Bongo Flava, Dully Sykes amesema hataki kuingilia ‘ugomvi’ wa Diamond na Alikiba kwa sababu wao ni biashara ya watu.

Muimbaji huyo anayefanya vizuri na ngoma Bombardier amesema Diamond na Alikiba ni kama klab za Simba na Yanga kusema zisiwepo zije timu nyingine ni kuua biashara.

“Sisi Tanzania Diamond na Alikiba ni biashara za watu na sitaki kuingilia kwa sababu utakuwa unaingilia kitu ambacho ni biashara unaweza kusema leo Simba na Yanga zisiwepo nani atakubali wakati watu ndio wanafanyia biashara,” amesema.

“Nafikiri siwezi kuingilia ugomvi wa Diamond na Alikiba, sitaki hata kuingilia ugomvi wao, Alikiba ni mdogo wangu nampenda, Diamond ni mdogo wangu nampenda, kwa upande wangu sioni tofauti zao,” amesisitiza.

Ameongeza tangu alipotaka kuwapatanisha kupitia wimbo na ikashindakana amekuwa akijiweka kando na mvutano wao.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.