Dudu Baya Amtupia Dongo Jux "Mimi Sio Msanii wa Kulia Lia Kama Jux Anayemlilia Vanessa" - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Dudu Baya Amtupia Dongo Jux "Mimi Sio Msanii wa Kulia Lia Kama Jux Anayemlilia Vanessa"

Msanii Dudu Baya amesema kuwa yeye sio msanii wa kulia lia kama Jux anayemlilia Vanessa.

Akiongea na Planet Bongo ya East Afrika Radio, Dudu Baya amesema yeye ni msanii anayebadilika kila wakati kulingana na kile kitu mashabiki wake wanataka.

"Mimi nabadilika kila wakati kulingana na mazingira, na ndo maana ukisikia nyimbo zangu kwa sasa ni kwaajili ya masela na sio watu wa kulia lia, kama wapo watu wanaotaka kulia lia wakamsikilize Jux anayemlilia Vanessa maana sio kila mtu kaachwa na Vanessa," amesema Dudubaya.

Dudubaya ni msanii wa Bongo Fleva aliyetamba zaidi katika miaka ya 2005 na nyimbo zake tofauti ikiwemo mpenzi, nakupenda tu na nyinginezo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.