Diamond Ashinda Tuzo, Alikiba na Vanessa Mdee Wamwagwa Tuzo za Soundcity 2017 - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Diamond Ashinda Tuzo, Alikiba na Vanessa Mdee Wamwagwa Tuzo za Soundcity 2017

Usiku wa kuamkia tarehe 13 Januari 2018 kumefanyika utoaji wa tuzo zinazoandaliwa na kituo cha runinga cha Soundcity. Tuzo hizo ambazo zimefanyika nchini Nigeria, kwa upande wa Tanzania tulikua tunawakilishwa na Vanessa Mdee, Alikiba na Diamond Platnumz Vanessa Mdee alikua kwenye kipengele cha Digital Artiste of the Year pamoja na wasanii wengine kama Davido Wizkid (NG), Cassper Nyovest (SA),AKA (S.),Yemi Alade (NG),Shatta Wale (GH) tuzo hiyo imeenda kwa msanii kutoka Nigeria Wizkid akiwa ndiyo msanii aliyeuza zaidi muziki wake kwa njia ya digitali.

Kwa upande mwengine Alikiba ameshindwa kutamba mbele ya Davido baada ya tuzo ya wimbo bora wa mwaka kwenda kwa Davido na wimbo wake wa If. Kwa upande mwingine Diamond Platnumz amefanikiwa kuchukua tuzo ya msanii bora wa kiume huku akiwamwaga Davido (NG),Runtown (NG),Sarkodie (GH),Navio (UG),2face Idibia (NG),Wizkid (NG),Shatta Wale (GH),Olamide (NG)

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.