Davido Atangaza Kuweka Hadharani Majina ya Watu Anaowadai - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Davido Atangaza Kuweka Hadharani Majina ya Watu Anaowadai

Unaweza ukasema ugumu wa mwezi Januari kwa upande wa uchumi ni kwa watu wakawaida lakini kumbe haipo hivyo hili ni janga hata kwa watu maarufu, Hii ni baada ya msanii wa muziki kutoka Nigeria, Davido kutangaza kuwa ataweka hadharani majina ya watu wote anaowadai kama hawatarudisha fedha zake kuanzia leo.

Davido kupitia ukurasa wake wa Snapchat amesema ametoa siku ya leo Jumatano kwa watu wote anaowadai ambao wapo jijini Lagos kutii amri hiyo la sivyo atatangaza majina hayo bila kuogopa ukubwa wa majina yao.

“Kupitia posti hiyo Davido amesema “Nitaweka orodha ya majina ya watu wote ninao wadai hapa Lagos, Watu wengi nimewakopesha pesa lakini hawataki kunilipa mimi sio serikali, Kama hutanilipa leo jina lako nitaliweka hadharani,” ameandika Davido.

Hata hivyo, watu wengi wanasema huenda hasira hizo zimekuja kutokana na Mamlaka ya mapato jijini Lagos kumtaka Davido atoe risiti za malipo ya kodi aliyolipa kwenye tamasha lake la 30 Bilioni Concert.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.