Darassa Afunguka Kuhusu Tetesi za Kutumia Dawa za Kulevya - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Darassa Afunguka Kuhusu Tetesi za Kutumia Dawa za Kulevya

Msanii wa muziki Bongo, Darassa amefunguka undani wa ukimya wake ambao umekuwa ukihusishwa na matumizi ya dawa za kulevya.

Rapper huyo ameimbia Clouds Fm hakuna kitu kama hicho ila ni maneno ambayo yanavumishwa kutokana na ukubwa wa jina lake lakini haonekani katika mitandao na katika maeneo ya starehe.

“Nimefanya vitu vikubwa sana, kila mtu atataka kuona nafanya makeke katika mitandao ya kijamii, niko na mwanamke huyu, nipo klabu lakini siyo kitu ambacho nakifanya,” amesema Darassa.

“Sasa kwa sababu sifanyi hivyo na nilikuwa nimefanya kazi kubwa sana basi nitakuwa nimechanganyikiwa kama siyo nimechanganyikiwa nitakuwa navuta unga lakini sio kitu ninachofanya,” amesisitiza.

Darassa ameongeza kuwa watu wanaogopa vitu vyenye ukimya wakijua mshindo wake huwa ni mkubwa hivyo wanazusha mambo kama hayo. Toka August 12 mwaka jana, 2017 Darassa hajaposti chochote katika mtandao wake wa Instagram.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.