Daktari wa White House Asema Afya ya Akili ya Trump ni Nzuri - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Daktari wa White House Asema Afya ya Akili ya Trump ni Nzuri

Bw Trump akimsalimia Dkt Jackson bbada ya uchunguzi Ijumaa

Rais Trump hajaonyesha dalili zozote za matatizo ya kiakili kufuatia uchunguzi wa kiafya na yuko la afya nzuri, daktari wa White House amesema.

"Sina wasi wasi wowote kuhusu afya ya akili ya Trump," Ronny Jackson alisema Jumanne.

Wiki iliyopita Trump alifanyiwa uchunguzi wa afya wa saa tatu, ambao ni wake wa kwanza tangu awe rais wa Marekani.

Hii ni baada ya kutolewa kitabu chenye utata kulichoeneza uvumi kuhusu afya ya kiakili ya Rais Trump.

Akiongea na waandishi wa habari wakati wa mkutano huko White House, Dkt Jackson alisema kuwa kwa jumla afya ya rais ni nzuiri.

"Anaendelea kufurahia moyo wenye afya na afya yote kwa jumla kutokana na kutovuta sigara na kutokunywa pombe," aliongzea.
Dr Jackson alisema hana wasi wasi na afya ya kiakili ya Trump

Hata hivyo Dkt Jakcson alisema kuwa Bw Trump, 71, atanufaika kwa kupunguza vyakula vyenye mafuta na mazoezi zaidi.

Siku ya Ijumaa rais alichunguzwa na madaktari wa kijeshi katika kituoa cha afya cha Walter Reed huko Bethesda, Maryland katika uchunguzi uliotajwa kuwa uliofanikiwa.

Kulingana na Michael Wolf ambaye ni mwandishi wa kitabu cha Fire and Fury: Inside the Trump White House, ni kuwa wafanyakazi wote wa White House walimuona Trump kama mtoto.

Trump alijibu kwa kusema kwa kitabu hicho kimejaa uongo huku naye waziri wa mashauri ya nchi za kigeni akikana madai kuwa afya ya rais ilikuwa inafeli.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.