Bill Nass Amuwezesha Uchebe Ili Kupambana na Nuh Mziwanda - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Bill Nass Amuwezesha Uchebe Ili Kupambana na Nuh Mziwanda

Bill Nass Amuwezesha Uchebe Ili Kupambana na Nuh Mziwanda
Msanii wa Bongo Fleva anayefanya vizuri katika game kwa sasa, Billnass amemtaka mume wa msanii Shilole, Uchebe kupambana pale inapobidi ndiyo maana ameamua kumzawadia vifaa vya mazoezi ili hata kupambana na Nuh Mziwanda pale ambapo inabidi.

Billnass ametoa kauli hiiyo wakati alipokuwa akiahidi zawadi kwa maharusi hao (Shilole na Uchebe) kwenye ukumbi uliofanyika Mikocheni, Jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia jana Jumatatu.

Msanii huyo amesema kwamba licha ya kuwa maharusi hao wamezawadiwa na kupewa ahadi mbalimbali yeye anafahamu mume wa msanii huyo anapenda sana michezo ya ngumi hivyo atampatia benchi la 'gym', punching bag na vifaa vinginevyo.

"Najua Mwanangu Ashraf (Uchebe) anapenda nini, anapenda michezo ya ngumi. Kwa kulitambua hilo mimi namzawadia mwanangu vifaa vya mazoezi ili aweze kufanya fitness. Ufanye mazoezi ya kupambana hata na kina Mziwanda, sisi watoto wakiume bana tunatakiwa kujilinda pale ambapo inabidi," Billnass.

Shilole na Uchebe walifanya sherehe ya harusi yao juzi Jumapili ambapo ilihudhuriwa na wasanii kibao na wengi wakitoa ahadi ya zawadi mbalimbali ikiwepo elimu na nyinginezo nyingi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.