Bill Nass Afunguka Kuhusu Ombi la Ndoa kwa Nandy - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Bill Nass Afunguka Kuhusu Ombi la Ndoa kwa Nandy

Bill Nass Afungu Kuhusu Ombi la Ndoa kwa Nandy
Msanii Bill Nass amejibu kauli ya Nandy aliposema kuwa anatamani angekuwa mke wake, na kusema kwamba ni kitu ambacho hakiwezekani ingawa anaheshimu hisia zake

Akizungumza na mwandishi wa EATV, Bill Nass amesema kwa sasa hawezi kujibu kwa mtazamo positive kwani kufanya hivo kutaharibu mahusiano yake ya sasa, lakini anaheshimu hisia za Nandy.

“Kwa comment yangu kwa sababu mtu ameelezea hisia zake kutokana labda na personality zangu, ila hanijui kiundani, siwezi kujibu in positive ingawa naheshimu hisia zake naheshimu alichokizungumza, lakini kutokana na mahusiano ambayo niko nayo siwezi kufanya move yoyote kwake, naheshimu mahusiano yangu, siwezi kucoment chochote ambacho hakitampendeza mwenzangu na hakitakuwa na mrejesho mzuri kwenye mahusiano yangu, lakini naheshimu hisia zake”, amesema Bill Nas.

Hivi karibuni msanii Nandy alinukuliwa na moja ya chombo cha habari akisema anatamani angekuwa mke wa Bill Nass kwani anamzimia msanii huyo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.