Belle 9: Ndoa Haiwezi Kunipoteza Kimuziki - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Belle 9: Ndoa Haiwezi Kunipoteza Kimuziki

Mwanamuziki anayetamba na Ngoma ya Mfalme, Abednego Damian ‘Belle 9’ ambaye hivi karibuni aliingia kwenye ndoa ameibuka na kusema hawezi kupotea kimuziki kisa kuoa kama wasanii wengi wanavyokuwa.

Akizungumza na Showbiz-Xtra, Belle 9 alisema, yeye ni msanii anayejiamini kwenye kazi zake hivyo hawezi kutetereka sababu ya ndoa, akashuka kimuziki kama ilivyotokea kwa wasanii wengine.

“Suala la kushuka kimuziki kisa ndoa sikubaliani nalo hata kidogo, hao wanaoshuka wanashuka kwa sababu zao binafsi, sidhani kama sababu ni ndoa, kwanza huyu mwanamke ninaye siku nyingi vipi nifeli baada ya kumuoa,” alisema.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.