Baba Levo Awapa Onyo Nuh Mziwanda na Nedy Music Kuhusu Shilole, ‘Mtagongwa Makofi’ - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Baba Levo Awapa Onyo Nuh Mziwanda na Nedy Music Kuhusu Shilole, ‘Mtagongwa Makofi’

Baada ya Shilole kufunga ndoa na mpenzi wake Uchebe, msanii Baba Levo amewataka Nuh Mziwanda na Nedy Music kukaa mbali na Shilole.

Nuh Mziwanda na Nedy Music waliwahi kutajwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Shilole kipindi cha nyuma.

Baba Levo amesema wasanii hao wasijewakatumia hicho kama kigezo cha kuendelea kwa karibu na Shilole kwani sasa ni mke wa mtu na endapo watafanya hivyo wataambulia makofi kutoka kwa uchebe.

“Hiki kilichotokea sasa hivi naomba Nuh Mziwanda Nedy Music sasa watulie Uchebe amekomaa atakupiga kofi, mtagongwa makofi biashara itaisha,” amesema.

“Na kuanzia sasa hivi Shilole atulie amuheshimu mume wake ambaye amekubaliana naye kuendesha maisha,” amesisitiza.

Usiku wa January 14 mwaka huu ndipo ilifanyika sherehe ya ndoa ya Shilole na Uchebe ambapo Baba Levo alikuwa MC wa shughuli hiyo.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.