Video: Bingwa wa Kupanda Majengo Marefu Afariki Dunia - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Video: Bingwa wa Kupanda Majengo Marefu Afariki Dunia

Mpanda mijengo mirefu ambaye ni maarufu sana nchini China amefariki akiwa anaonyesha moja ya ujuzi wake hatari.

Wu Yongning alikuwa amejizolea maelfu ya mashabiki kwenye mtandao ya kijamii wa Weibo, kutokana na video zake fupi za kutisha akiwa juu ya majengo marefu bila ya kuchukua tahadhari zozote za kiusalama.Wasi wasi uliwaingia mashabiki wake wakati ambapo aliacha kuchapisha video zake mwezi Novemba mwaka huu.

Sasa imeibuka kuwa alifariki baada ya kuanguka kutoka jumba la ghorofa 62 kwenye mji wa Changsha.

Vyombo vya habari nchini China vinasema kuwa alikuwa akishiriki kwenye mchezo wa kushinda pesa nyingi.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.