Ujumbe wa Diamond kwa Mwanaye Wawakera Wanawake, Atuhumiwa Kuwadhalilisha Wanawake - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Ujumbe wa Diamond kwa Mwanaye Wawakera Wanawake, Atuhumiwa Kuwadhalilisha Wanawake

Ujumbe wa Diamond kwa Mwanaye Wawakera Wanawake... Atuhumiwa Kuwadhalilisha Wanawake
Msanii Diamond Platnumz anayetamba na Ngoma ya Sikomi ameingia matatani baada ya  watu mbalimbali kumtuhumu kuwadhalilisha wanawake kupitia ujumbe wake aliouandika katika ukurasa wake wa Instagram.

Ujumbe huo ambao ulikuwa ni maalum kwa ajili ya kumtakia heri ya kuzaliwa mtoto wake wa kiume, Nillan, ulimtaka mtoto huyo akue salama ili aje awatumie wanawake vyovyote atakavyo kwa sababu  anajituma ili amwandalie pesa ya kutumia vyovyote atakavyo atakapokuwa mkubwa.

“Nasemaje! Kua Uje kuwatembezea Baba... We swala la Kutafta ela niachie mie... Jukumu lako ni moja tu, Kupita nao.....Happy 1st Year Lanny!!!” Unasomeka ujumbe huo wa Diamond.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.