Shilole: Sijaingia Kwenye Ndoa Kucheza - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Shilole: Sijaingia Kwenye Ndoa Kucheza

Staa wa bongo fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amefunguka kuwa, watu wasimfikirie ameamua kuingia kwenye ndoa kama maonyesho bali amedhamiria kwenda kuwa mke anayestahili kuwa mfano wa kuigwa.

Mrembo huyo anayesumbua na wimbo wa Hatutoi Kiki, alisema kuwa anajua wazi watu wengi wanamuhesabia siku za uhusiano wao kuvunjika kama ilivyo kwa mastaa wengine, lakini kwa jinsi alivyodhamiria kutulia kwenye ndoa atawashangaza walimwengu.

“Najua wazi watu watakuwa wananihesabia siku ndani ya ndoa yangu lakini ukweli ni kwamba nitawashangaza watu wengi na sina sababu ya kuacha kuwa mke bora na mwenye heshima kwa mume,” alisema.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.