Shamsa Ford, Babu Tale Wawajia Juu Tanesco Baada ya Ukataji wa Umeme - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Shamsa Ford, Babu Tale Wawajia Juu Tanesco Baada ya Ukataji wa Umeme

Mwanadada kutoka bongo muvi Shamsa Ford pamoja na meneja wa Diamond Babu Tale kwa nyakati tofauti wamejikuta wakiwashambulia Tanesco kwa kutumia akaunti zao za Instargram kutokana na tatizo linaloendelea nchini la kukatika mara kwa mara kwa umeme

Shamsa Ford Ameandika "Jamani mmezidi basi mtupe taarifa mapema kabla ya kukata huo umeme wenu. Nimenunua vinyama vyangunimeweka kwenye friji ili zinisaidie taratibu mwisho wa siku zimeharibika... jamaniii daaa mnatuumiza"

kwa upande wa babu Tale Ameandika "kama mmeanza kutoa huduma ya mgao si bora mseme tu kuliko hiki kinachoendelea tena kwa siku kama ya leo ya sikukuu . Tatizo mpo pekeyenu ingekuwa wanaosambaza umeme wapo zaidi  ya mmoja hii huduma isingekuwa inalegalega kama uduma za simu vile maana Afrika nzima Tanzania pekee ndio matumizi ya simu yapo kwa bei nafuu" 

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.