Penzi la Rayvanny na Fahyma Bado Lipo Sawa, Kumbe Ilikuwa Kiki Tu - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Penzi la Rayvanny na Fahyma Bado Lipo Sawa, Kumbe Ilikuwa Kiki Tu

Hivi karibuni kulikuwa na drama za hapa na pale kuwa msanii wa muziki Bongo, Rayvanny ameachana na Baby Mama wake, Fahyma lakini hilo limekuja kuonekana kutokuwa na ukweli wowote mara baada ya msanii huyo kutoa video ya wimbo wake ‘Safari’ ambapo ndani yupo Fahyma.

Licha ya video hiyo kuthibitisha kuwa penzi bado lipo pale pale, Rayvany pia amepigilia msumari katika hilo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram amendika; “Sikukupata kwa Bahati Mbaya Kwanini Nikuache kwa Makusudi NAKUPENDA MAMA,”.

Katika hatua nyingine mashabiki wa Rayvanny amekuwa na maoni tofauti kuhusiana na drama hiyo na jinsi ilivyomalizika. Haya ni baadhi ya maoni yao kutoka kwenye mtandao wa Instagram;

ney_faidaIzo Kiki za kuachana ni ujinga mtupu kwan uwez kutoa wimbo mpk Kiki za ivo mxiew

kilaveelizabethnice kama umelijua hilo maan jua huyo niwa thaman kuliko vyote coz yeye ndio anae jua maumiv yak na fulah yak usimuache mkeo kisa manen ya watu kaka au kwa ugomvi kumbuka wewe ni binadam na yeye wote hamja kamilika vumilianeni saw kaka@rayvanny mpenda San@fahy_rayvanny

dkng6267Ile ilikua kiki na tulishtukaaa mapemaa

katotopureUjue siku atakufa mtu na tujue ni kiki

carrymastorySasa kiki zakuachana za nn Akili kama za darasa la pili

faizahremix@rayvanny ngoma kali sana kakangu..ila uache kutuchezea akili najua kabisa hamkuwa mumeachana ilikuwa kiki ya hii ngoma na kwakweli tuneisearch sana youtube. Mihela utapata ila naomba na pia mm unisaidie…@faizah kenya.

Wimbo wa Safari ambayo Rayvanny amemshirikisha Nikki wa Pili amechukua baadhi ya vionjo kutoka kwenye wimbo wa msanii wa dansi Husein Jumbe ‘Mapenzi ya Siri’.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.