Nandy Amshukuru Naibu Spika kwa Kuusifia Wimbo wake wa Kivuruge - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Nandy Amshukuru Naibu Spika kwa Kuusifia Wimbo wake wa Kivuruge

Msanii wa muziki wa bongo fleva Nandy, amesema anamshukuru Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa pongezi alizompa, kwani ni kitu ambacho hakikutarajia.

Nandy amesema kuwa ni kitu cha faraja kuona anapongezwa na kiongozi mkubwa serikalini, hivyo kimempa faraja.

“Nimefurahi kwa sababu ni mtu ambaye ananisapoti sana, na imenipa faraja sana kwani sikutarajia, kwa sababu mi nilitumiwa kwenye group nikaiona, basi nikampigia simu nikaongea naye nikamshukuru”, amesema Nandy.

Jana Naibu Spika Tulia Ackson alipost kwenye instagram yake akimpongeza Nandy kwa jitihada zake anazozifanya kwenye kazi yake ya sana ya muziki.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.