Lulu Diva: Sina Kinyongo na Wala Sijaumia Belle 9 Kuoa - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Lulu Diva: Sina Kinyongo na Wala Sijaumia Belle 9 Kuoa

Msanii anayefanya poa kwenye ulimwengu wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ ambaye kipindi cha nyuma aliwahi kuweka wazi hisia zake kwamba anamzimikia msanii mwenzake, Abednego Damian ‘Belle 9’ ambaye amefunga ndoa ya siri siku chache zilizopita amesema kuwa, hana kinyongo na wala hajaumia na jambo hilo

Akizungumza na Mikito Nusunusu baada ya kuenea minong’ono ya wambea wa jiji kwamba kitendo cha Belle 9 kufunga ndoa kitakuwa kimemuumiza mrembo huyo alisema, hajaumia hata kidogo sababu kwa sasa Belle 9 ni rafiki yake wa karibu wala hawazi tena mambo ya mapenzi.

“Ni kweli niliwahi kuweka wazi hisia zangu kwamba namzimikia enzi hizo, lakini hayo yalipita Belle 9 tunaheshimiana kama marafiki tu, pia nashukuru alinialika kwenye harusi yake lakini mambo yalinibana nikashindwa kwenda, kikubwa nampongeza kufunga pingu za maisha,”alisema.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.