Lulu Diva Adaiwa Kumeza Vidonge Vya Kubadili Ngozi - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Lulu Diva Adaiwa Kumeza Vidonge Vya Kubadili Ngozi

Muuza nyago kwenye video za Bongo ambaye pia ni mwanamuziki, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ anadaiwa kutumia vidonge vya kubadili ngozi ambapo mwili wake kwa sasa unaonekana mweupe tofauti na zamani ulivyokuwa.

Kwa mujibu wa chanzo, Lulu Diva kabla hajaingia katika kuuza nyago na muziki alikuwa na ngozi ya maji ya kunde lakini kwa sasa imebadilika kwa kiasi kikubwa na kuwa mweupe tii.

“Ukiangalia hata picha zake za zamani na sasa utaona utofauti. Ametumia kidonge na ndiyo maana amebadilika ngozi mwili mzima,” kilidai chanzo.

Star Mix ilimtafuta Lulu Diva kujua ukweli na alipopatikana alifunguka; “Mambo ya kumeza vidonge mbona yamepitwa na wakati kabisa jamani, hii ni ngozi yangu asilia sema tu nilikuwa sijapata vitu vya kuipendezesha.”

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.