Jacqueline Wolper Kuolewa Hivi Karibuni - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Jacqueline Wolper Kuolewa Hivi Karibuni

Msanii wa filamu Bongo na mwanamitindo, Jacqueline Wolper huenda akafunga ndoa hivi karibuni mara baada ya kuweka wazi mipango yake ya kwenda kumtambulisha mpenzi wake kwa wazazi wake.

Licha ya kutomtaja muhusika, Wolper ameeleza kuwa mpenzi wake huyo ameridhia suala hilo kwani naye pia alikuwa akilihitaji toka mwanzo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wolper ameandika mengi kuhusiana na hilo ila hapa tumenukuu haya machache;

Wewe ni mwanaume ambae umejitoa ili tu niwe wako,umetaka tufike mbali kwanza kabla ya mambo mengine (uwende kwa wazazi, (NDOA) pamoja na kwamba mahusiano yangu ya nyuma yalikuwa yana misukosuko mingi ila umemthamini Jacq. Nilipotoka niliteswa sana na mapenzi yaani usaliti, dharau, kukosa na mapenz ya dhati.

Pamoja ya kuwa pia alishatokea mmakonde na kunipeleka mapaka Mtwara na matembele nikachuma na wanakijiji kunipokea na kupikia familia na kutambulishwa kwa wazazi lakini sikufanikiwa kufikia hatua hii ambayo umefika, umenijali na umenisikiliza nilipokwambia sihitaji mtu bali nahitaji future husband.


Pia ameongeza kuwa katika mahusiano amejifunza kunyamaza bila kuyaweka hadharani na siku ya leo ndipo anatarajia kumtambulisha nyumbani kwao, Moshi na taratibu nyingine kama mahari kufuata.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.