Dr. Shika: Simfahamu Babu Seya - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Dr. Shika: Simfahamu Babu Seya

Dr. Luis Shika amesema hamjui mwanamuziki Babu Seya na Papii Kocha ambao wametoka jela kwa msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli alioutoa katika maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanganyika.

Dr. Shika amesema wakati Babu Seya anaingia nchini Tanzania yeye alikuwa nje ya nchi hivyo hajawahi kumuona lakini anafahamu nyimbo zake ambazo aliwahi kuimba.

”Simfahamu Babu Seya, wakati anaingia nchini tayari nilishaondoka nchini muda mrefu, lakini nafahamu nyimbo zake ile aliyoimba baba na mwana tunaimba na kucheza ndio haswa naifahamu vizuri”, amesema.

Pia Dr. Shika amempongeza Rais Magufuli kwa kuwatoa wafungwa mbali mbalimbali na kutumia vizuri fursa ya uongozi kama mkuu wa nchi. ”Nampongeza Rais Magufuli kwa tukio hili la kuwatoa wafungwa na kuwapa uhuru wakaanze maisha yao upya”, ameongeza.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.