Barnaba 'Nahitaji Wasanii Watatu Wa Kike Tu' - BongoSwaggz.Com

Advert

Breaking News

Barnaba 'Nahitaji Wasanii Watatu Wa Kike Tu'

Msanii wa muziki Bongo, Barnaba amesema mwakani anahitaji kuanza kuchukua wasanii kwa ajili ya label yake ila wa kike pekee.

Muimbaji huyo ameiambia 5 Selekt, EATV kuwa anahitaji wasanii wa kike watatu kwani wa kiume tayari wapo wengi katika game.

“Mimi label yangu ni changa hata mwaka jana nilisema nitatambulisha wasanii, mwakani nitamtoa (Mula) na nitaanza kuchukua chapa nyingine na in fact nimesema nahitaji wasanii wa kike sana, nahitaji wa kike watatu tu” amesema Barnaba.

“Kwa hiyo wa kiume atabaki Mula pekee na ni sababu ya msingi sana wanaume tupo wengi sana, halafu nimeamua kufanya hivyo kwa sababu mimi ni mwandishi mara nyingi nyimbo zangu zinawiana kwa mabinti na nimeamua kuja hivyo, am sure mtu kama Diamond ameshasaidia sana” ameongeza.

Download App Yetu MPYA  >> BOFYA HAPA << Tukutumie Habari na Burudani Zote FASTA Kila Siku !

No comments

TOA MAONI YAKO HAPO CHINI.